Msaada wa Wakristo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Msaada wa Wakristo (kwa Kilatini: Auxilium Christianorum) ni sifa mojawapo ya Bikira Maria katika Kanisa Katoliki.
Yohane Krisostomo alikuwa wa kwanza kutumia jina hilo mwaka 345.
Baadaye, Ukristo ulipoatharishwa na uenezi wa Waislamu, waumini walimkimbilia Maria kwa jina hilo ili kupata msaada wa sala zake. Hasa mwaka 1571, Waturuki walipokaribia kuteka Ulaya, Papa Pius V aliombea jeshi la Kikristo kwa kuagiza sala ya Rozari hadi ushindi ulipopatikana katika mapigano ya Lepanto.
Yohane Bosco ndiye aliyeeneza zaidi heshima hiyo.
Mtaguso wa pili wa Vatikano, katika hati juu ya Kanisa (61, 62), ulitaja jina hilo ukieleza umama wa Maria[1].