Mkuzi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mkuzi ni kata ya Wilaya ya Muheza katika Mkoa wa Tanga, Tanzania.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 8,785 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 7,948 [2]
Msimbo wa posta ni 21419.
Wenyeji wa kata ya Mkuzi ni Wabondei. Asilimia kubwa ya Wabondei ni wakulima wa machungwa, mahindi, mpunga na ndizi, pia wanafuga mbuzi, kuku, bata na ng'ombe wa maziwa.
Kata ya Mkuzi ina vijiji vinne ambavyo ni Mkuzi, Mafere, Mindu na Lunguza. Inasemekana kata ilianzia kwenye kijiji cha Mafere wakati wa biashara ya utumwa. Baadhi ya watumwa waliokuwa dhaifu sana waliachwa hapo na baadaye walipona na kuendelea na maisha hapo. Ikumbukwe kuwa hapo Mafere ndipo ilipopita njia ya kusafirisha watumwa kwenda wilaya ya Pangani ambapo watumwa walisafirishwa kwa njia ya maji kwenda maeneo mengine.
Jina la Mkuzi lilikuwepo tangu zamani za ukoloni wa Wajerumani na ndio waliojenga kanisa kubwa kuliko yote katika kata hiyo. Kanisa hilo lilijengwa kwa kutumia mawe makubwa na bado linatumika kwa ibada, halina ufa wowote.