Melito wa Sardi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Melito wa Sardi (kwa Kigiriki Μελίτων Σάρδεων, Melíton Sárdeon) (alifariki mwaka 180) alikuwa askofu wa mji huo karibu na Smirna katika rasi ya Anatolia (leo nchini Uturuki).
Pamoja na kwamba maisha yake hayajulikani vizuri, katika Ukristo wa zamani aliheshimiwa sana: Jeromu, akizungumzia Agano la Kale lilivyokubaliwa na Melito kuwa Neno la Mungu, aliripoti maneno ya Tertullian kwamba waamini wengi wa Afrika Kaskazini walimhesabu kama nabii.
Hata katika karne za kati jina lake liliendelea kutumika katika uandishi wa vitabu ili vithaminiwe zaidi.
Leo anaheshimiwa na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.
Sikukuu yake inaadhimishwa hasa tarehe 1 Aprili, lakini pia 31 Agosti[1].