mji wa Mpumalanga, Afrika Kusini From Wikipedia, the free encyclopedia
Mbombela (awali: Nelspruit) ni mji mkuu wa jimbo la Mpumalanga katika Afrika Kusini. Uko kando ya mto Crocodile (mamba) takriban km 330 upande wa mashariki wa Johannesburg na km 60 upande wa magharibi wa mpaka wa Msumbiji.
Mbombela | |
Mahali pa mji wa Mbombela katika Afrika Kusini |
|
Majiranukta: 25°28′12″S 30°58′48″E | |
Nchi | Afrika Kusini |
---|---|
Majimbo | Mpumalanga |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 695,913 |
Mji wenyewe una wakazi 695,913 pamoja na vitongoji vilivyojenga wakati wa siasa ya apartheid viko mbali kidogo ni KaNyamazane, Msogwaba, Mpakeni na Matsulu.
Mbombela ni kitovu cha huduma na biashara kwa mazingira yenye kilimo kingi; kuna pia viwanda vinavyoshughulikia mazao kama machungwa, malimau, maembe, jozi na ndizi.
Kuna kituo cha reli pamoja na uwanja wa ndege. Kuna utalii kutokana na wageni wa hifadhi ya taifa ya Kruger iliyo karibu.
Mbombela ilikuwa mahali mojawapo pa kombe la dunia la soka mwaka 2010.