mji mkubwa nchini Afrika Kusini From Wikipedia, the free encyclopedia
Johannesburg (inayojulikana pia kama iGoli) ni jiji kubwa katika nchi ya Afrika Kusini. Ni mji mkuu wa jimbo la Gauteng.
Jiji la Johannesburg | |||
| |||
Mahali pa mji wa Johannesburg katika Afrika Kusini |
|||
Majiranukta: 26°11′24″S 28°2′24″E | |||
Nchi | Afrika Kusini | ||
---|---|---|---|
Majimbo | Gauteng | ||
Tovuti: www.joburg.org.za |
Mji ulianzishwa 4 Oktoba 1886 ukakua haraka baada ya kupatikana kwa dhahabu. Siku hizi ni kitovu cha kiuchumi wa Afrika Kusini na makao ya soko la hisa kubwa katika Afrika.
Japokuwa johannesburg ni mji mkubwa lakini sio miongoni mwa miji mikuu mitatu ya Afrika Kusini lakini mahakama ya katiba inakaa hapa.
Pia kuna jengo lililosheheni maofisi kubwa kuliko yote barani Afrika ambalo linaitwa Carlton Centre lenye ghorofa 50 kuna pia jengo refu kabisa barani afrika linaloitwa Hillbrow Tower (mita 270 au maghorofa 90).
Karibu theluthi moja ya wakazi wa jiji la johannesburg huishi katika eneo la Soweto ambalo ni mtaa maarufu ulioengwa nje ya jiji asilia kwa ajili ya wafanyakazi Waafrika wakati wa Apartheid (siasa ya ubaguzi wa rangi). Jozi kama inavyojulikana na wengi ni moja kati ya miji mikubwa duniani iliyoendelea(kujengeka) sehemu ambako hakuna mto,ziwa ama bahari ufukwe..! Imehaririwa na Selemani Mkonje
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika Kusini bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Johannesburg kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.