Masange
From Wikipedia, the free encyclopedia
Masange ni kata ya Wilaya ya Kondoa katika Mkoa wa Dodoma, Tanzania, yenye postikodi namba 41710[1].
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 6,556 [2]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 5388 [3] waishio humo.
Baadhi ya vijiji vya kata ya Masange vyenye shule ya msingi ni Masange yenyewe, Mkekena, Kwayondu, Kandaga na Itololo. Asilimia kubwa za wakazi wa kata ya Masange ni Warangi.