Malkia wa Sheba
From Wikipedia, the free encyclopedia
Malkia wa Sheba (kwa Kiebrania מַלְכַּת שְׁבָא malkaṯ shəḇāʾ; kwa Kiarabu: ملكة سبأ) ni mhusika anayetajwa kwa mara ya kwanza katika Biblia ya Kiebrania (1 Fal 10:2, 2 Nya 9). Katika taarifa hiyo, anaongoza msafara wa zawadi za thamani kwa Mfalme Sulemani wa Israeli. Taarifa hiyo imepitia ufafanuzi wa kina wa Kiyahudi, Kiislamu na Kiethiopia. Imekuwa chanzo cha hadithi zilizoenea katika nchi za Mashariki ya Kati. [1]
Wanahistoria wa leo wanaona "Sheba" kuwa ufalme ule unaoitwa pia "Saba" kusini mwa Uarabuni kwenye maeneo ya Yemen leo. Kuwepo kwa malkia huyo kunabishaniwa kati ya wanahistoria. [2]