Majarra ya Mara
From Wikipedia, the free encyclopedia
Majarra ya Mara (ing. Andromeda Galaxy, inajulikana pia kama Messier 31, M31 au NGC 224) ni majarra kubwa iliyo karibu zaidi na majarra yetu ya Njia Nyeupe. Umbali wake na Dunia ni takriban miakanuru milioni 2.5. Inaonekana katika eneo la kundinyota la Mara linaloitwa "Andromeda" kwa jina la kimataifa na hii ni chanzo cha jina lake. Ni sehemu ya kundi janibu la majarra pamoja na Njia Nyeupe, Mawingu ya Magellan na takriban majarra 40 nyingine.
Ukweli wa haraka
Kundinyota | Mara (Andromeda) |
Mwangaza unaonekana | +3.44 |
Umbali (miakanuru) | milioni 2.5 |
Mwangaza halisi | -21.5 |
Masi M☉ | 1.5×1012 |
Majina mbadala | Messier 31, M31, NGC 224 |
Funga
Ina mwangaza unaoonekana wa mag 3.4 na hivyo inaonekana kama nyota hafifu kwa mtazamaji. Hivyo ni kiolwa cha anga cha mbali kinachoonekana bila darubini.