Njia Nyeupe (pia "mkokoto wa kondoo za Sumaili" [1]; kwa KiingerezaMilky Way) ni mlia mpana wa nyota nyingi unaoonekana angani wakati wa usiku kama wingu jeupe linalong`aa.
Njia nyeupe jinsi inavyoonekana usiku (picha ilipigwa jangwani pasipo na machafuko wa nuru)
Galaksi yetu jinsi inaaminiwa kuonekana vile kama tunaiangalia kutoka juu; picha ya galaksi ya mbali yenye mikono miwili ya parafujo
Galaksi yetu inafanana na hii NGC 4565 tunayoona kutoka pembeni kabisa. Tunatambua vizuri jinsi gani mlia wa nyota zake unanenepa kidogo kwenye kitovu penye nyota nyingi.