From Wikipedia, the free encyclopedia
Lamadi ni mji mdogo na kata ya Wilaya ya Busega katika Mkoa wa Simiyu, Tanzania, yenye postikodi namba 39507 [1].
Mji wa Lamadi umepakana na Ziwa Viktoria upande wa Magharibi, Pori la Akiba Kijereshi na Kata za Lutubiga na Mkula upande wa Mashariki, Wilaya ya Bunda upande wa Kaskazini na Kata ya Kalemela upande wa Kusini. Mji wa Lamadi ufikika kwa barabara za kitaifa ambazo ni Barabara ya Mwanza - Musoma, pamoja na Barabara ya Shinyanga, Bariadi - Lamadi.
Mitaa yake ni Itongo, Makanisani, Majengo, Msekula Road, Mwalukonge, Kisesa na vijiji vitatu ambavyo ni Lukungu, Mwabayanda na Kalago (Mwabulugu Lakeshore).
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 44,146 [2]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 22,062 waishio humo.[3].
Wakazi walio wengi ni wa makabila ya Wasukuma, Wajita, Wakurya, Wazanaki na Waha.
Mji wa Lamadi ni maarufu kwa biashara, uvuvi, utalii, kilimo na ufugaji.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.