Lalibela, Ethiopia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Lalibela ni mji unaopatikana kaskazini mwa Ethiopia. Ni mmoja kati ya miji mitakatifu nchini humo.
Mji huu ni wa pili kwa utakatifu ukifuatia ule wa Aksum, na pia ni patakatifu kwa ajili ya kufanyia hija kwa wakazi wengi wa nchini Ethiopia.
Tofauti na mji wa Aksum, watu wengi katika mji wa Lalibela kwa ujumla ni Wakristo Waorthodoksi wa Mashariki. Lalibela ilikusudiwa kuwa Yerusalemu mpya kama matokeo ya mji wa Yerusalemu kuchukuliwa na Waislamu. Hata majina kadhaa katika kanisa la Lalibela yametokana na majengo mbalimbali katika mji wa Yerusalemu.
Likiwa linapatikana katika ukanda wa Semien Wollo (Semien Wollo Zone) wa kabila la Amhara au Kilil mita 2.500 juu ya usawa wa bahari.
Kutokana na takwimu za serikali, mwaka 2005, mji wa Lalibela ulikadiriwa kuwa na idadi ya watu wapatao 14,668 ambao kati yao, 7,049 ni wanaume na 7,619 ni wanawake. [1]. [2]
Katika Lalibela pia kunapatikana uwanja wa ndege wa Lalibela unaoitwa Lalibela Airport (Kodi ya ICAO HALL, IATA LLI), soko kubwa, shule na hospitali moja.