Kupalizwa Maria katika sanaa
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kupalizwa Maria katika sanaa ni aina ya michoro na sanamu za Bikira Maria inayokusudiwa kuonyesha fumbo linaloadhimishwa na Kanisa Katoliki katika sherehe ya Kupalizwa Mbinguni, tarehe 15 Agosti.
Imani kuhusu fumbo jilo ilijitokeza katika sanaa muda mrefu kabla ya Papa Pius XII kutangaza (1950) dogma ya kwamba, mwishoni mwa maisha ya Bikira Maria, huyo Mama wa Yesu alichukuliwa mbinguni mwili na roho.