From Wikipedia, the free encyclopedia
Kisiju ni kata ya Wilaya ya Mkuranga katika Mkoa wa Pwani, Tanzania yenye postikodi namba 61513.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 8,101 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 12,113 [2] walioishi humo.
Kitovu chake ni mji mdogo ambao ni ni bandari kwenye pwani ya Bahari Hindi na kisiwa cha Kwale inahesabiwa ndani ya eneo lake. Kisiju iko takriban kilomita 100 kusini kwa Dar es Salaam upande wa kaskazini wa delta ya mto Rufiji.
Eneo la mji wenyewe lina takriban hektari 8. Ni bandari kubwa kati ya Dar es Salaam na Kilwa. Biashara yote kutoka na kwenda visiwa vya Kwale na Koma inapita bandari yake pamoja na sehemu za bidhaa zinezopelekwa Mafia. Kuna huduma ya mabasi kwenda Dar es Salaam.
Eneo la Kisiju pamoja na visiwa limekaliwa tangu zamani sana. Wataalamu wa akiolojia waligundua mabaki ya makazi ya kibinadamu tangu karne ya 1 BK [3]
Mabaki ya bidhaa yamepatikana tangu karne ya 6 na hii inadokeza kuwa eneo la Kisiju lilikuwa kwenye vituo vya kwanza vya biashara ya pwani iliyokuwa chanzo cha utamaduni wa Waswahili.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.