Kipwe
Jenasi ya ndege / From Wikipedia, the free encyclopedia
Vipwe au gongo futa ni ndege wa jenasi Dryoscopus katika familia Malaconotidae. Wanatokea Afrika kusini kwa Sahara tu. Ndege hawa ni weusi kwa utosi, mgongo na mabawa na weupe chini na kwa kiuno. Domo lao ni jembamba kwa kulinganishwa na spishi nyingine za familia hii. Hula wadudu na invertebrata wengine. Hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe mtini au kichakani na jike huyataga mayai 2-3.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi ...
Kipwe | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kipwe kiuno-cheupe | ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Funga