Kipunjabi cha Magharibi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kipunjabi cha Magharibi (pia Kilahnda) ni lugha ya Kihindi-Kiulaya nchini Pakistan na Uhindi inayozungumzwa na Wapunjabi. Mwaka wa 2015 idadi ya wasemaji wa Kipunjabi cha Magharibi nchini Pakistan imehesabiwa kuwa watu zaidi ya tisini milioni. Pia kuna wasemaji 1,910,000 nchini Uhindi (2007). Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kipunjabi cha Magharibi iko katika kundi la Kiaryan. Wengine hutumia jina la Kilahnda kujumlisha lugha hii pamoja na Kisaraiki, Kihindko cha Kusini na cha Kaskazini, Kipahari-Potwari na Kikhetrani.