Kinakara
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kinakara (au Kinakkara) ni lugha ya Kigunwinyguan nchini Australia inayozungumzwa na Wanakara katika jimbo la Northern Territory. Katika sensa ya mwaka 2006, idadi ya wasemaji wa Kinakara ilihesabiwa kuwa watu hamsini tu. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kinakara kiko katika kundi la Kiburarran pamoja na Kiburarra, Kidjeebbana na Kiguragone.