Kiburarra
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiburarra ni lugha ya Kigunwinyguan nchini Australia inayozungumzwa na Waburarra katika jimbo la Northern Territory. Katika sensa ya mwaka 2006, idadi ya wasemaji wa Kiburarra ilihesabiwa kuwa watu 1070. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiburarra kiko katika kundi la Kiburarran pamoja na Kidjeebbana, Kiguragone na Kinakara.