Kidjeebbana
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kidjeebbana ni lugha ya Kigunwinyguan nchini Australia inayozungumzwa na Wagunavidji katika jimbo la Northern Territory. Katika sensa ya mwaka 2006, idadi ya wasemaji wa Kidjeebbana ilihesabiwa kuwa watu 240. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kidjeebbana kiko katika kundi la Kiburarran pamoja na Kiburarra, Kiguragone na Kinakara.