Kiguragone
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiguragone ni lugha ya Kigunwinyguan nchini Australia inayozungumzwa na Waguragone katika jimbo la Northern Territory. Mwaka wa 2011, idadi ya wasemaji wa Kiguragone ilihesabiwa kuwa watu sitini tu. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiguragone kiko katika kundi la Kiburarran pamoja na Kiburarra, Kidjeebbana na Kinakara.