Kidatu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kidatu ni kata ya Wilaya ya Ifakara Mjini katika Mkoa wa Morogoro, Tanzania, yenye Postikodi namba 67508.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/1/1a/Kidatu.jpg/220px-Kidatu.jpg)
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 27,463 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 32,589 [2] walioishi humo.
Iko kando ya hifadhi ya taifa ya milima ya Udzungwa iliyopo upande wa kaskazini karibu na mto Ruaha Mkuu, pale inapotoka milimani na kuingia katika tambarare ya Kilombero. Milima hiyo inasaidia kuongeza uchumi wa taifa kwa sekta ya utalii hapa nchini.
Inapakana na hifadhi ya wanyama ya Selous upande wa kusini.