Kamusi Kuu ya Kiswahili
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kamusi Kuu ya Kiswahili (KKK) ni kamusi ya lugha ya Kiswahili iliyotolewa na Baraza la Kiswahili la Taifa la Tanzania mwaka 2015 baada ya maandalizi ya miaka minne[1].
Toleo hilo limechapishwa na kusambazwa na Longhorn. Mwaka 2017 ilipatikana pia kama app ya android kwa ajili ya mitambo ya simujanja[2].