Simujanja
From Wikipedia, the free encyclopedia
Simujanja ni aina ya rununu ambayo inafanya mambo mengi kuliko simu nyingine ya kawaida.[1] Zinafanya kazi kama tarakilishi, lakini hiki ni chombo kinachobebeka na kidogo cha kutosha katika mkono wa mtumiaji.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/b/bf/Samsung_Foldable_Smartphone.jpg/640px-Samsung_Foldable_Smartphone.jpg)
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/c/c2/HTC_Desire_Z_overview.jpg/640px-HTC_Desire_Z_overview.jpg)
Matumizi yake ni pamoja na:
- Kutuma na kupokea barua pepe, matini mafupi, picha na jumbe za media kadhaa
- Kuorodhesha mawasiliano
- Vifanyizi vya kikokotoo, fedha, king'ora, n.k.
- Kuvinjari intaneti kwa kutumia kivinjari cha simu
- Kucheza michezo mbalimbali
- Bluetooth
- GPS
- Wi-Fi
Kwa sababu simujanja ni kama tarakilishi ndogo, zinaweza kuendeshwa kwa kutumia mifumo ya uendeshaji kama vile Apple iOS na Android - itategemea na mahitaji ya chombo chenyewe. Lakini vilevile wengine wanatumia Windows Phone au BlackBerry OS.[2]