Junipero Serra
From Wikipedia, the free encyclopedia
Junipero Serra, O.F.M. (jina la kiraia lilikuwa Miquel Josep Serra i Ferrer; Petra, Majorca, Hispania, 24 Novemba 1713 - misheni ya San Carlos Borromeo de Carmelo, California, Hispania Mpya, leo nchini Marekani, 28 Agosti 1784) alikuwa mtawa, padri na mmisionari wa Kanisa Katoliki.
Alianzisha misheni moja katika Baja California na nyingine 9 kati ya 21 za kwanza kati ya San Diego na San Francisco, Marekani. Walengwa wakuu wa misheni hizo walikuwa Waindio, ambao aliwainjilisha kwa lugha zao pamoja na kutetea kwa nguvu haki za maskini, bila kujali matatizo na magumu mengi[1].
Alitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa mwenye heri tarehe 25 Septemba 1988, halafu na Papa Fransisko kuwa mtakatifu tarehe 23 Septemba 2015.[2]
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 28 Agosti[3] au 1 Julai [4].