Julius Caesar
Jenerali wa Kirumi, kiongozi wa serikali na Dikteta wa mwisho / From Wikipedia, the free encyclopedia
Gaius Julius Caesar (tamka gayus yulius kaesar[1] - 100 - 44 KK) alikuwa kiongozi wa kisiasa na wa kijeshi wa Roma ya Kale.
Anakumbukwa hasa kwa mafanikio mbalimbali yanayoonekana kuathiri dunia hadi leo.
Baadhi ya mafanikio hayo ni:
- Kama kiongozi wa kijeshi aliteka Gallia (leo: Ufaransa) na kuifanya jimbo la Kiroma. Kutokana na hiyo lugha ya Kifaransa ni karibu sana na Kilatini, lugha ya Roma ya Kale.
- Waroma wa Kale walimheshimu kushinda viongozi wote waliomfuata au kutangulia akatangazwa kuwa mungu. Jina lake lilipata kuwa neno kwa ajili ya cheo cha watawala wa Kiroma waliomfuata. Kutokana na badiliko hilo la jina "Caesar" kuwa cheo, lugha mbalimbali zilipokea cheo hicho kama vile Kijerumani ("Kaiser"), Kirusi ("Tsar") na Kiswahili ("Kaisari" - kutokana na neno la Kijerumani).
- Aliunda kalenda ambayo imekuwa msingi wa kalenda ya kimataifa leo (Kalenda ya Juliasi). Kwa heshima yake, mwezi wa saba unaitwa Julai.
- Katika historia ya Roma alifunga kipindi cha Jamhuri - kilichofuata ni Dola la Roma aliloliwekea misingi.