![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/5/58/James_Morrison_at_Dances_With_Films_World_Premiere%252C_June_1_2014.jpg/640px-James_Morrison_at_Dances_With_Films_World_Premiere%252C_June_1_2014.jpg&w=640&q=50)
James Morrison
From Wikipedia, the free encyclopedia
James Paige Morrison (amezaliwa tar. 21 Aprili 1954) ni mwigizaji wa filamu na tamthilia kutoka nchini Marekani. Alizaliwa mjini Bountiful Utah, ni mtoto wa kiongozi wa maofisa,[1] na alikulia mjini Anchorage, Alaska, Marekani.
James Morrison | |
---|---|
![]() | |
Amezaliwa | James Paige Morrison 21 Aprili 1954 (1954-04-21) (umri 70) Bountiful, Utah, Marekani |
Ndoa | Riad Galayini (1995–hadi leo) |
Tovuti rasmi |
Katika vipindi vya TV, Morrison amepata kuonekana katika mfululizo wa Frasier, The X-Files, JAG, Murder She Wrote, The West Wing na Six Feet Under.
Hivi karibuni amepata kushika nafasi katika mfululizo wa TV wa 24. Humo alicheza kama mkurugenzi wa CTU na alitumia jina la Bill Buchanan. Alianza kama nyota mgeni katikati ya msimu wa nne (2005), na akaja kuwa katika orodha ya wahusika wakuu katika msimu wa tano, sita, na saba (2006, 2007, 2009), hadi pale uhusika wake ulipokuja kuuawa.
Yeye na mkewe wanaishi mjini Los Angeles na mtoto wao wa kiume, Seamus, ambaye alizaliwa mnamo mwaka wa 1999.