Iridi
From Wikipedia, the free encyclopedia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Iridi ni elementi haba na metali adimu yenye namba atomia 77 katika jedwali la elementi. Alama yake ni Ir. Inahesabiwa katika kundi la Platini. Kati ya metali zote inaathiriwa kidogo kabisa na mmenyuko wa kikemia.
Iridi (iridium) | |
---|---|
Jina la Elementi | Iridi (iridium) |
Alama | Ir |
Namba atomia | 77 |
Uzani atomia | 192,217 |
Ugumu (Mohs) | 6.5 |
Kiwango cha kuyeyuka | 2739 K (2466 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 4701 K (4428°C) |
Asilimia za ganda la dunia | 1·10-7 % |
Iridi ilitambuliwa na Smithson Trennant mwaka 1803 pamoja na metali ya Osmi. Alijaribu kuyeyusha madini ya platini katika asidi akakuta metali hizo mbili. Alichagua jina la "iridium" kutokana na neno la Kigiriki "iridios" kwa sababu ya rangi nyingi za chumvi zake. Tabia ya kutomeyuka kulisababisha uteuzi wa iridi kwa aloi ya mita asilia.
Iridi ni kati ya metali haba kabisa duniani. Hutokea pamoja na platini au kama madini ya mchanganyiko pamoja na Osmi. Nchi zenye akiba za Iridi ni hasa Afrika Kusini, Urusi (milima ya Ural), Amerika ya Kaskazini na ya Kusini, Japani, Borneo na Tasmania.
Hutumiwa ndani ya aloi za metali ikiongeza ugumu wa aloi hizo. Mwaka 2007 kilogramu 3,700 za iridi zilitumiwa duniani; kati ya hizo takriban kilogramu 780 ziliingia katika vifaa vya umeme kama plagi za cheche kwenye injini za mwako ndani; 1,100 kg zikatumiwa kwa elektrodi.
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Iridi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.