Ifigenia wa Ethiopia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Ifigenia wa Ethiopia (kwa Kigiriki: Ἰφιγένεια, Ifigeneia[1]) alikuwa mwanamke wa karne ya 1 ambaye maisha yake yanasimuliwa na kitabu Golden Legend [2].
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/8/89/Santa_Ifig%C3%AAnia_-_MG%2C_s%C3%A9c._XVIII.jpg/130px-Santa_Ifig%C3%AAnia_-_MG%2C_s%C3%A9c._XVIII.jpg)
Humo tunasikia kwamba alikuwa bikira aliyeongokea Ukristo na kuwekwa wakfu kwa Mungu kwa njia ya Mathayo Mtume, alipokuwa anaeneza Injili huko "Ethiopia," kwa maana ya eneo kusini kwa Bahari Kaspi,[3] yaani Mesopotamia au Armenia (Colchis).[note 1][note 2]
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 21 Septemba[10][11][12] au 16 Novemba[13][14]