Gregori wa Tours
From Wikipedia, the free encyclopedia
Gregori wa Tours (Clermont-Ferrand, Auvergne, 30 Novemba 538 hivi [1] - Tours, 17 Novemba 594[2]) alikuwa mwanahistoria na askofu wa Tours katika Ufaransa wa leo[3].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 17 Novemba[4].