![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/3/3d/Graphite-233436.jpg/640px-Graphite-233436.jpg&w=640&q=50)
Grafati
From Wikipedia, the free encyclopedia
Grafati (kwa Kiingereza: graphite) ni umbo la pekee la elementi kaboni linalopatikana kwa fuwele za pembesita.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/3/3d/Graphite-233436.jpg/320px-Graphite-233436.jpg)
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/8/8f/0.5mm_Pacer.jpg/640px-0.5mm_Pacer.jpg)
Grafati ni umbo linalotokea kiasili ikiwa ni umbo thabiti zaidi la kaboni katika hali sanifu. Ikiathiriwa na joto kali na shinikizo kubwa inageuka kuwa almasi.
Inatokea kiasili katika fomu hii na ni aina ngumu zaidi ya kaboni chini ya hali ya kawaida. Chini ya shinikizo kubwa na joto hubadilika kuwa almasi .
Matumizi ya grafati yapo katika penseli na ulainishaji. Grafati ni kipitishi kizuri cha joto na umeme. Uwezo huu unaipa nafasi muhimu katika teknolojia ya elektroniki kama vile elektrodi, beteri na paneli za sola.
Grafati hutokea ndani ya miamba metamofia ambako inachimbwa ama katika mashimo ya wazi au chini ya ardhi. Akiba kubwa za grafati zilitambuliwa katika Wilaya ya Ruangwa (Mkoa wa Lindi) na kampuni ya Uranex iliyo mali ya Magnis Energy Technologies ya Australia imepata laiseni ya kuchimba grafati kwenye eneo la kilomita za mraba 30[1].