Epafrodito
From Wikipedia, the free encyclopedia
Epafrodito (kwa Kigiriki: Ἐπαφρόδιτος, yaani "Mpendevu"[1][2]) ni Mkristo wa karne ya 1 anayetajwa katika Agano Jipya[3] kama mjumbe wa kanisa la Filipi kwa kumhudumia Mtume Paulo kifungoni (Fil 2:25-30; pia 4:18). Akiwa huko aliugua, hivyo Paulo alipoona amepona akamrudisha Filipi kwa shukrani.
Paulo alimuita ndugu na mwenzi katika kazi na katika mapambano (ya utume).
Inasemekana baadaye akawa askofu.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 22 Machi[4] au 30 Machi[5].