Mjini Ghana From Wikipedia, the free encyclopedia
Elmina ni mji wa Jamhuri ya Ghana, Mkoa wa Kati. Elmina iko kwenye mwambao wa Ghuba ya Guinea ambayo ni pwani ya kusini ya Ghana, takriban kilomita 12 upande wa magharibi wa Cape Coast.
Elmina ilifikiwa na Wareno mara ya kwanza mnamo mwaka 1471 walipokuta biashara ya dhahabu iliyoendeshwa baina ya wenyeji na wafanyabiashara Waarabu. Hivyo wakaita mji "mina" yaani mgodi kwa sababu walichukua hapa dhahabu. Wareno walijenga kituo wakaendelea kushiriki katika biashara hiyo na mwaka 1481 walijenga Ngome ya Elmina (Castelo de São Jorge da Mina). Ngome hiyo ilikuwa makao makuu ya Wareno kwenye pwani ya Afrika Magharibi hadi kutwaliwa na Waholanzi mnamo 1637 walioendelea kuitumia hadi mwaka 1872 walipoiuza kwa Waingereza.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.