Editha
From Wikipedia, the free encyclopedia
Editha wa Wilton (jina asili Eadgyth limerahisishwa pia kama Edith au Ediva; Kemsing, Kent, Uingereza, 961 hivi[1] – Wilton Abbey, 15 Septemba 984) alikuwa binti wa mfalme Edgar wa Waangli ambaye tangu utotoni aliishi kama mmonaki katika abasia ya Wilton, hivi kwamba alionekana si kuacha malimwengu, bali kutoyafahamu kabisa [2].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu bikira.
Sikukuu yake huadhimishwa na Wakatoliki na Waanglikana tarehe 16 Septemba[3][4].