Brid wa Kildare
From Wikipedia, the free encyclopedia
Brid wa Kildare au Brigid wa Ireland (kwa Kikelti Naomh Bríd; kwa Kilatini Brigida; Faughart, Dundalk, 453 hivi - Kildare, 524 hivi[1][2][3]) ni mmojawapo kati ya watakatifu wasimamizi wa Ireland (pamoja na Patrick na Kolumba).[4]
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/0/09/Stbrigid.jpg)
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/b/b1/Saint_Non%27s_Chapel_-_Fenster_3_St.Bride.jpg/640px-Saint_Non%27s_Chapel_-_Fenster_3_St.Bride.jpg)
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/b/bd/Saint_Brigid%27s_cross.jpg/640px-Saint_Brigid%27s_cross.jpg)
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/0/0a/Gross_stmartin_brigida_von_kildare.jpg/640px-Gross_stmartin_brigida_von_kildare.jpg)
Anatajwa kama mmonaki, abesi, na mwanzilishi wa monasteri kadhaa za kike, ikiwemo ile maarufu ya Kildare, ambayo ni kati ya zile za kale zaidi huko Ireland.
Pia mchango wake katika kuendeleza uinjilishaji wa kisiwa hicho uliofanywa na Patrick wa Ireland unaheshimiwa sana hadi leo.
Anahesabiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waanglikana kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Februari[5], pamoja na ya Dar Lugdach, mwanafunzi wake aliyerithi mamlaka yake.