Bikira Maria katika sanaa anajitokeza sana (hasa katika uchoraji na uchongaji) tangu zamani sana (karne ya 2 na ya 3) kulingana na maendeleo ya heshima ya Wakristo kwake[1] hasa baada ya Mtaguso wa Efeso (431) uliokubali jina "Mama wa Mungu" kuwa sahihi[2].

Thumb
Salus Populi Romani, picha takatifu ya karne ya 5 au ya 6 hivi.

Kwa kuwa ukuu wake mwenyewe unamtegemea tu Yesu Mwanae, mara nyingi wako pamoja (hasa katika Ukristo wa Mashariki), lakini pengine anaonyeshwa peke yake.

Michoro yake ya kale zaidi inapatikana katika makatakombu ya Roma[3], ingawa inasimuliwa (hasa Mashariki) kuwa Mwinjili Luka alimchora Bikira Maria akiwa hai.

Namna za kumchora baadaye zilitofautiana sana upande wa Ukristo wa Magharibi wakati wa Renaissance (Duccio, Leonardo da Vinci, Michelangelo, Raphael, Giovanni Bellini, Caravaggio na Rubens) na baadaye (Salvador Dalí na Henry Moore), kumbe upande wa Mashariki wasanii waliendelea kuzingatia vielelezo vilivyokubalika kimapokeo.

Muhammad alipotakasa Kaaba kwa kuondoa sanamu na michoro yote, aliokoa ile ya Bikira Maria na mtoto Yesu na Abrahamu[4][5][6][7].

Michoro

Sanamu

Michoro midogo

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Tanbihi

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.