Augusto
From Wikipedia, the free encyclopedia
Augusto alikuwa Kaisari wa kwanza wa Dola la Roma kuanzia mwaka 27 KK hadi 14 BK. Jina lake la kiraia lilikuwa Gaius Octavius. Alizaliwa Italia tarehe 23 Septemba 63 KK.
Octavius alikuwa mpwa wa Julius Caesar aliyempenda kijana huyo na kumteua kama mrithi katika wasia wake.
Historia ya Augusto ina vipindi viwili:
- kipindi cha kwanza kinamwonyesha mwanasiasa kijana ambaye ni mkali akitafuta kulipiza kisasi kwa uuaji wa mjomba wake na kushinda maadui wote katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.
- kipindi cha pili kinamwonyesha mtawala wa Dola la Roma mwenye upole na hekima anayefaulu kujenga Roma upya katika kipindi kirefu cha amani na maendeleo.