![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/9/96/DD_Frauenkirche_Aaron.jpg/640px-DD_Frauenkirche_Aaron.jpg&w=640&q=50)
Aroni
From Wikipedia, the free encyclopedia
Aroni (au Harun; kwa Kiebrania: אַהֲרֹן, ′aharon; kwa Kiarabu: هارون, Hārūn, kwa Kigiriki: Ἀαρών, Aaron; alifariki juu ya Mlima Hor, leo nchini Yordani, karne ya 13 KK) alikuwa kaka wa Musa. Dada yao aliitwa Mariamu.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/9/96/DD_Frauenkirche_Aaron.jpg/640px-DD_Frauenkirche_Aaron.jpg)
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/6/63/GoldCalf.jpg/640px-GoldCalf.jpg)
Walikuwa watoto wa Amram na wa shangazi yake Jokebed, wote wa kabila la Lawi, taifa la Israeli.
Ndiye aliyepakwa mafuta na Musa kuwa kuhani mkuu wa kwanza wa dini yao, na makuhani wote waliofuata walitakiwa kuwa wanaume waliotokana naye kwa kuzaliwa upande wa baba[1].
Wanae waliitwa Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.