Ambrosi Edwadi Barlow
From Wikipedia, the free encyclopedia
Ambrosi Edwadi Barlow, O.S.B. (Manchester, Uingereza, 1585 ā Tyburn, London, 10 Septemba 1641[1]) alikuwa Mkristo wa Kanisa la Anglikana kabla hajajiunga na Kanisa Katoliki mwaka 1607.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/3/31/Saint-ambrose-edward-barlow.jpg/200px-Saint-ambrose-edward-barlow.jpg)
Baada ya kuhamia Ufaransa, aliingia seminari kwa kengo la kurudi kwao kufanya uchungaji usioruhusiwa na serikali. Baadaye alijiunga na monasteri ya Wabenedikto (1615) na kupewa daraja ya upadri (1617).
Hapo alirudi Uingereza alipofanya uchungaji kwa siri kwa miaka 24 katika eneo la Lancaster akiimarisha waumini katika imani na moyo wa ibada[2].
Alikataa kukimbia hata baada ya mwili wake kupooza na dhuluma ya mfalme Charles I kutisha zaidi. Hivyo alikamatwa akiwa anahubiri kwenye sikukuu ya Pasaka na, baada ya kufungwa, aliuawa kikatili sana[3]
Papa Pius XI alimtangaza mwenye heri tarehe 15 Desemba 1929, halafu Papa Paulo VI tarehe 25 Oktoba 1970 alimtangaza kuwa mtakatifu mfiadini pamoja na wenzake 39[4][5].