From Wikipedia, the free encyclopedia
Alexander Donald Gwebe Nyirenda (aliizaliwa Karonga, Malawi [1] 2 Februari 1936 )[2] ni askari wa Tanzania aliyepata umaarufu kwa kupandisha bendera ya Tanganyika huru juu ya Mlima Kilimanjaro.
Alexander Nyirenda | |
Stempu yenye Picha Luteni Alexander Nyirenda akipandisha bendera ya Taifa mara baada ya Tanganyika Kupata Uhuru. | |
Amezaliwa | 2 Februari 1936 Karonga, Malawi |
---|---|
Amekufa | 2 Desemba 2008 (umri 72) Saratani ya Umio |
Nchi | Tanzania |
Anafahamika kwa | Kwa Kusimiki Mwenge wa Uhuru na Kupandisha bendera ya Taifa Katika kilele cha mlima Kilimanjaro |
Kazi yake | Mwanajeshi |
Mwajiri | Jamuhuri ya Muungano Wa Tanzania |
Elimu | Mchikichini, Malangali, Chuo cha Kifalme cha Kijeshi cha Sandhurst |
Mwenza | Hilda Simkoko |
Watoto | 5 |
Alisoma katika shule ya msingi ya Mchikichini jijini Dar es Salaam. Alipomaliza elimu ya msingi alichaguliwa kuendelea na masomo ya Upili katika shule ya wavulana ya Malangali iliyoko mkoani Iringa na baadae akaendelea na elimu hiyo Mkoani Tabora na kuhitimu masomo yake mwaka 1957.
Alichaguliwa kuendelea na amali ya kijeshi na mwaka 1958 akachaguliwa kwenda nchini Uingereza katika chuo cha kijeshi kilichoitwa Sandhurst kwa masomo ya uafisa kadeti.
Baada ya kumaliza masomo yake alirejea nchini Tanganyika na kujiunga na "Kings African Rifles" mwaka 1960.
Tarehe 9 Desemba mwaka 1962 Nyirenda aliingia kwenye vitabu vya historia kwa kupanda mlima Kilimanjaro mpaka kileleni na kusimika bendera ya Tanganyika baada ya kupata uhuru kutoka kwa wakoloni na nchi kuwa chini ya Julius Kambarage Nyerere[3].
Aliondoka jeshini Mwezi wa nane mwaka 1964 kama Luteni Kanali.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.