Karonga

From Wikipedia, the free encyclopedia

Karonga

Karonga ni mji kaskazini mwa Malawi kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa. Ni makao makuu ya Wilaya ya Karonga inayopakana na Tanzania.

Thumb
Mji Mkongwe, Karonga. Kaskazini mwa Malawi

Mnamo mwaka 2018, Karonga ilikadiriwa kuwa na wakazi 61,609.

Jiografia

Karonga iko kwenye mwinuko wa mita 478 juu ya UB kwenye ufuo wa magharibi wa Ziwa Nyasa.[1]

Historia

Zana za zama za mawe za kale na mabaki ya viumbehai waliofanana na binadamu wa kwanza zinaonyesha kwamba maeneo ya Karonga yalikaliwa mapema sana.

Ugunduzi huo ulikuwa katika eneo la uchimbaji wa Malema km 10 (mi 6) kutoka Karonga.

Wakati wa karne ya 19 kabla ya mwaka 1877 Karonga ilifahamika ngome ya Mlozi aliyekuwa mfanyabiashara wa watumwa.[2] Mnamo 1883 kituo cha biashara cha Uingereza kilifunguliwa huko ambacho kiliendelea kikawa chanzo cha mji wa leo. [2] Mvumbuzi Mwingereza Harry Johnston alivamia ngome ya Mlozi na kumaliza utawala wake. [2] Kuanzia hapo Karonga ikawa kituo muhimu cha biashara na kilimo. [2]

Mnamo Desemba 2009 eneo hilo lilipata mfululizo wa matetemeko ya ardhi.

Tazama pia

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.