From Wikipedia, the free encyclopedia
Zakayo (kwa Kigiriki Ζακχαῖος, Zakkhaios; kwa Kiebrania זכי, "safi", "asiye na kosa"[1]) alikuwa mtozaushuru tajiri mjini Yeriko aliyepata umaarufu kupitia Injili ya Luka ambayo katika sura ya 19 inasimulia alivyoongoka alipomkaribisha Yesu Kristo nyumbani mwake kwa kumuahidia atawagawia mafukara nusu ya mali yake na kuwarudishia mara nne watu aliowadhulumu kitu.
Kwa kumtafuta mtu kama huyo, aliyetazamwa na Wayahudi kama mpotevu kutokana na kazi yake haramu kwao, Yesu alidhihirisha kwamba alikuja kutafuta waliopotea, wakiwemo matajiri wanaokubali kuachana na uroho ili kujali shida za wengine. Hiyo ni mada muhimu katika Injili hiyo.
Zakayo ni mfano wa kuigwa na matajiri wa leo. Matajiri kwa kawaida yao ni watu wanaojali faida kwa gharama yoyote ile, kwa kupokonya cha maskini ili wafaidike wao. Wanajihalalishia kuwa ni haki yao kuwa matajiri na kuwasahau maskini. Wanachojali ni pesa iingie mifukoni mwao na si vinginevyo.
Inasemekana baadaye alikuwa askofu wa kwanza wa Kaisarea ya Palestina[2]..
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 20 Agosti au 27 Agosti au 20 Aprili au tarehe nyingine[3].
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.