From Wikipedia, the free encyclopedia
Yosefu Pham Thong Ta (1800-1859) ni mmojawapo kati ya Wakristo wafiadini wa Vietnam waliouawa kwa ajili ya imani yao huko Vietnam katika karne ya 17, 18 na 19 (1625–1886).
Wanatajwa pia kama Watakatifu Andrea Dũng-Lạc na wenzake 116.
, Pamoja na Dominiko Pham Thong (1780-1859) na mwanae Luka Thin Viet Pham (1819-1859) aliteswa vikali na hatimaye kufia dini huko Nam Dinh, Vietnam Kaskazini kwa kuwa walikataa kukanyaga msalaba.
Kwa nyakati tofauti, Papa Leo XIII, Papa Pius X na Papa Pius XII waliwatangaza kuwa wenye heri, halafu Papa Yohane Paulo II aliwaunganisha katika kuwafanya watakatifu wafiadini tarehe 19 Juni 1988.
Sikukuu yao huadhimishwa kwa pamoja kila tarehe 24 Novemba, ila ya kwake ni tarehe 13 Januari[1].
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.