From Wikipedia, the free encyclopedia
Yohane Payne (Peterborough, 1532 – Chelmsford, 2 Aprili 1582) alikuwa padri wa Uingereza aliyeuawa kwa ajili ya imani Katoliki wakati wa dhuluma za serikali ya nchi hiyo yenye Ushirika wa Anglikana kama dini rasmi.
Mwaka 1574 alijiunga na seminari huko Douai, Ufaransa, na miaka miwili baadaye alipata upadrisho[1]. Siku chache baadaye akarudi Uingereza pamoja na Cuthbert Mayne ili kufanya utume.
Alipokamatwa mara ya kwanza alilazimika kurudi Ufaransa, lakini mwaka 1579 alirudi tena Uingereza akafanya utume kwa mwaka mmoja unusu tena halafu alinyongwa kwa kisingizio cha usaliti dhidi ya malkia Elizabeti I; watu waliohudhuria walifaulu kuzuia asiraruliwe vipandevipande [2] kama mapadri wengine [3].
Alitangazwa mwenye heri na Papa Leo XIII tarehe 29 Desemba 1886 na mtakatifu na Papa Paulo VI tarehe 25 Oktoba 1970[4].
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.