Bonde la Wafalme (kwa Kiarabu: وادي الملوك‎ wadi al-muluk) ni bonde la huko Misri ya Kusini. Kuanzia karne ya 16 KK hadi karne ya 11 KK mafarao na wakubwa wao walizikwa huko katika makaburi yaliyochongwa kwenye miamba.[1] [2]

Thumb
Mahali pa bonde katika Milima ya Theban, magharibi mwa Nile, Oktoba 1988 (Rangi nyeusi ni mto Nile na kanda la mashamba yanayomwagiliwa, mshale mwekundu unaonyesha eneo)

Bonde hilo liko kwenye ukingo wa magharibi wa Mto Nile likitazama mji wa Luxor na mahekalu yake. [3] Baadhi ya wafalme waliozikwa huko ni:

Bonde hilo ni mojawapo kati ya maeneo maarufu ya akiolojia duniani. Mnamo 1979 limepokewa katika orodha ya Urithi wa Dunia, pamoja na makaburi yote ya eneo la Thebes ya kale (Theban Necropolis) [4] Uchunguzi, uchimbaji na uhifadhi unaendelea bondeni ukiongozwa na mamlaka ya Hifadhi ya Urithi wa Utamaduni ya Misri. Kituo kipya cha watalii kimefunguliwa hivi karibuni.

Thumb
Bonde la Wafalme likiangaliwa kutoka kaskazini.

Jiolojia na hali ya hewa

Thumb
Matabaka ya bonde hilo.

Kuna mvua kidogo ya mwaka mzima katika sehemu hii ya Misri, lakini kuna mafuriko ya nadra ambayo hutokea ghafla katika bonde. Yaliwahi kupeleka tani za matope na mawe ndani ya makaburi yaliyokuwa wazi.

Marejeo

Kusoma zaidi

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.