Remove ads
From Wikipedia, the free encyclopedia
Utaifa ni itikadi ya mtu kupenda taifa lake kupita kiasi, hata kudharau watu wa mataifa mengine. Hivyo ni tofauti na uzalendo unaomfanya mtu apende nchi yake kwa kutambua mema mengi aliyopata kutoka kwake. [1]
Mara nyingi unajitokeza pia kama dharau kwa wananchi walio tofauti na kawaida kwa utamaduni, lugha n.k.
Katika ngazi ya chini, tunakuta ukabila.
Bendera ya taifa, wimbo wa taifa na alama nyingine za utambulisho ni muhimu katika kuchochea uzalendo, lakini mara nyingine zinachangia utaifa.[2][3][4][5]
Elimunafsia inaeleza kwamba pendo kwa taifa linatokana na haja ya kuhusiana na wengine, lakini ni tofauti na mapendo mengine, k.mf. pendo kwa dini au kwa mchumba.
Kwa vyovyote ukomavu unadai mtu ajali wenzake asiwaone kama maadui kwa sababu tu ni tofauti naye.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.