Ulaya ya Magharibi ni sehemu ya magharibi ya bara la Ulaya. Kuna maelezo tofauti ni nchi zipi ambazo ni sehemu ya kanda hilo. Maelezo hutofautiana kutokana na njia mbalimbali za kuangalia sehemu hiyo: kwa maana ya kijiografia, kihistoria, kisiasa au kiutamaduni.
Kanda la kijiografia
Kama kanda la kijiografia mara nyingi nchi zifuatazo zinahesabiwa kuwa Ulaya ya Magharibi:
Mpangilio wa Umoja wa Mataifa
Umoja wa Mataifa umepanga kanda hili tofauti, hasa kwa kuhesabu Ufalme wa Muungano upande wa Ulaya ya Kaskazini, lakini pia kwa kuingiza Ujerumani, Austria na Uswisi ambazo zinahesabiwa mara nyingi kama sehemu ya Ulaya ya Kati wakati mpangilio wa UM hauna Ulaya ya Kati.
Ulaya ya Magharibi kihistoria katika karne ya 20
Wakati wa "vita baridi" Ulaya ya Magharibi ilimaanisha mara nyingi nchi zote za Ulaya zilizofungamana na upande wa magharibi yaani Marekani na NATO dhidi nchi za kikomunisti zilizoshikamana na Umoja wa Kisovyeti.
Wikiwand in your browser!
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.