Bunzi ni nyigu wa familia Sphecidae walio na kiuno chembemba na kirefu sana (petiole).

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Bunzi
Thumb
Bunzi akibeba mdudu wa jamii ya senene (Sphex argentatus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Hymenoptera (Wadudu wenye mabawa mangavu)
Nusuoda: Apocrita (Hymenoptera wenye kiuno chembamba sana)
Familia ya juu: Apoidea (Apocrita kama nyuki)
Familia: Sphecidae
Latreille, 1802
Ngazi za chini

Nusufamilia 4, jenasi 19, 9 katika Afrika ya Mashariki:

  • Ammophilinae André, 1886
    • Ammophila Kirby, 1798
    • Eremnophila Menke, 1964
    • Eremochares Gribodo, 1883
    • Hoplammophila De Beaumont, 1960
    • Parapsammophila Taschenberg, 1869
    • Podalonia Fernald, 1927
  • Chloriontinae Fernald, 1905
    • Chlorion Latreille, 1802
  • Sceliphrinae Ashmead, 1899
    • Chalybion Dahlbom, 1843
    • Dynatus Lepeletier, 1845
    • Penepodium Menke, 1976
    • Podium Fabricius, 1804
    • Sceliphron Klug, 1801
    • Trigonopsis Perty, 1833
  • Sphecinae Bohart & Menke, 1963
    • Chilosphex Menke, 1976
    • Isodontia Patton, 1880
    • Palmodes Kohl, 1890
    • Prionyx Vander Linden, 1827
    • Sphex Linnaeus, 1758
    • Stangeella Menke, 1962
Funga

Nyigu wa nusufamilia Eumeninae katika familia Vespidae huitwa bunzi pia. Halafu kuna bunzi-buibui wa familia Pompilidae.

Maelezo

Bunzi wa Sphecidae wana kiuno chembamba na kirefu. Hata fumbatio ni nyembamba na ndefu kiasi kwa kawaida. Nyigu hao ni weusi au buluu au weusi pamoja na njano au nyekundu. Urefu wao ni mm 15-40.

Mwenendo

Wengi wa bunzi hawa huchimba vishimo kwenye mchanga au kujenga chumba kimoja au kadhaa kwenye matundu yaliyopo. Walakini, spishi nyingine huunda vyumba vya nje kwa matope au hata kwa sandarusi. Kama bunzi wa Eumeninae, huweka viwavi, mabuu au buibui waliopoozwa kwenye vyumba kabla ya kutaga yai katika kila kimoja. Spishi fulani hutaga mayai kadhaa kwenye chumba kimoja kikubwa. Spishi kadhaa za Sceliphrinae hata zinaonyesha aina sahili ya ujamii, ambapo majike kadhaa hujenga vyumba karibu na kila kimoja na kuvilinda pamoja. Walakini, kila jike huwapea mwenyewe mayai yake chakula.

Spishi za Afrika ya Mashariki[1]

  • Ammophila africana
  • Ammophila argyrocephala
  • Ammophila barbarorum
  • Ammophila bechuana
  • Ammophila beniniensis
  • Ammophila calva'
  • Ammophila clypeolineata
  • Ammophila crassifemoralis
  • Ammophila curvistriata
  • Ammophila dolichocephala
  • Ammophila dolichodera
  • Ammophila dubia
  • Ammophila fischeri
  • Ammophila kenyensis
  • Ammophila malickyi
  • Ammophila pseudodolichodera
  • Ammophila punctatipes
  • Ammophila ressli
  • Ammophila rubiginosa
  • Ammophila rubripes
  • Ammophila saussurei
  • Ammophila schalleri
  • Ammophila theryi
  • Ammophila tuberculiscutis
  • Ammophila vulcania
  • Ammophila zambiensis
  • Ammophila zetteli
  • Chalybion clypeatum
  • Chalybion japonicum
  • Chalybion kenyae
  • Chalybion laevigatum
  • Chalybion mochii
  • Chalybion parvulum
  • Chalybion sommereni
  • Chalybion spinolae
  • Chlorion maxillosum
  • Isodontia longiventris
  • Isodontia pelopoeiformis
  • Isodontia stanleyi
  • Parapsammophila ponderosa
  • Parapsammophila testaceipes
  • Podalonia canescens
  • Prionyx crudelis
  • Prionyx funebris
  • Prionyx indus
  • Prionyx kirbii
  • Prionyx subfuscatus
  • Prionyx viduatus
  • Sceliphron fossuliferum
  • Sceliphron spirifex
  • Sphex argentatus
  • Sphex bohemanni
  • Sphex fumicatus
  • Sphex haemorrhoidalis
  • Sphex incomptus
  • Sphex lanatus
  • Sphex neavei
  • Sphex nigrohirtus
  • Sphex observabilis
  • Sphex satanas
  • Sphex stadelmanni
  • Sphex tomentosus

Picha

Marejeo

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.