Elimu ya sekondari (shule za upili), katika mifumo ya kisasa ya elimu ulimwenguni, huchukua kipindi cha pili cha elimu rasmi ambayo hutokea wakati wa ujana wa wanafunzi.

Thumb
Wasichana katika shule ya sekondari huko Iraq.

Mfumo huu hutofautiana na masomo ya msingi ambayo ni ya lazima, ni ya jumla na yanayofanana. Yale ya shule za upili ni teule na ya hiari. Shule hizi hujulikana kama sekondari, shule za upili, shule za kati, vyuo au shule za ujuzi wa kitaalamu kulingana na kipindi au mfumo unaofuatwa.

Maana ya dhana hizi hutofautiana kutoka mfumo mmoja hadi mwingine. Mpaka kamili kati ya elimu ya msingi na ya upili hutofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine. Tofauti hizi zipo hata katika nchi, lakini kwa jumla hutokea kati ya mwaka wa saba na wa kumi wa kusoma.

Elimu ya sekondari hutokea katika umri wa ujana. Nchini Marekani na Kanada, elimu ya msingi na sekondari kwa pamoja hurejelewa kama elimu ya K-12 na nchini Nyuzilandi, elimu hii hurejelewa kama elimu ya miaka 1-13. Azma ya elimu ya sekondari ni kutoa maarifa ya kawaida, kutayarisha wanafunzi kwa elimu ya juu au kuwafunza kazi moja kwa moja.

Tunapaswa kujitahidi katika kuhamasisha elimu ya sekondari kwani huwezesha kufikia chuo kikuu.

Historia

Barani Ulaya, shule za sarufi au akademia zilikuwepo hata katika miaka ya 1500. Shule za umma au zile za kulipa karo au hata shule za ufadhili na za wakfu zina historia ndefu zaidi.

Elimu ya sekondari iliibuka nchini Marekani mwaka 1910 na ilisababishwa na kuwepo kwa biashara kubwa na maendeleo ya teknolojia viwandani. Ili kuafikia mahitaji ya kazi, shule za upili zilijengwa na mtaala uliolenga maarifa ya kazi za ofisi na za sulubu ukazinduliwa. Hii ilibainika kuwa njia ya manufaa kwa mwajiri kwani uimarishaji wa huduma za kibinadamu uliwafanya waajiriwa kuwa madhubuti kazini na kushusha gharama kwa waajiri, huku waajiriwa wakinufaika na mishahara minono ikilinganishwa na waliokuwa na elimu ya msingi pekee.

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.