From Wikipedia, the free encyclopedia
Washia (pia: Shi'a; kutoka Kiarabu:شيعة[1]) ni dhehebu katika Uislamu (Kiarabu: الإسلام). Kufuatana na makadirio mbalimbali kati ya asilimia 10 na 20 za Waislamu wote hufuata Shia na wengine walio wengi ni Wasunni.
Sehemu ya mfululizo wa makala juu ya |
Imani na ibada zake |
Umoja wa Mungu |
Waislamu muhimu |
Abu Bakr • Ali |
Maandiko na Sheria |
Qur'an • Sunnah • Hadithi |
Historia ya Uislamu |
Historia |
Tamaduni za Kiislamu |
Shule • Madrasa |
Tazama pia |
Uislamu na dini nyingine |
Lakini katika nchi za Uajemi, Azerbaijan, Iraki, Bahrain, Yemen, Omani na Lebanoni Washia ndio kundi kubwa.
Tofauti kubwa kati ya madhehebu mawili hayo ni juu ya suala la uimamu au ukhalifa baada ya Mtume; hata hivyo, wana tofauti juu ya masuala mengine ya kiitikadi na hukumu pia.
Waislamu wa shia wanaamini kwamba hakuna uwongo au makosa katika Qur'an na imebakia bila kubadilika tangu kuteremshwa kwake. Hadithi inajumuisha hotuba na matendo ya Mtume na Maimamu yanayopitishwa kwetu kwa njia ya maandishi kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
Neno Shia linatokana na Kiarabu shiá't ali (شیعته علی) yaani "chama cha Ali" likimaanisha kundi la wafuasi wa Ali ibn Abu Talib aliyekuwa mkwe wake Mtume Muhammad na familia yake. Dhehebu hili linashikilia na kuamini kwamba Mtume alimteua Ali kama Wasii wake (Khalīfa) na Uimamu (mafundisho ya Shia) (kiongozi wa kiroho na kisiasa) baada yake.[2] Uteuzi huo ulifanyika katika tukio la Ghadir Khumm, lakini alizuiwa kumrithi Muhammad kama kiongozi wa Waislamu kama matokeo ya chaguo lililofanywa na baadhi ya masahaba wengine wa Muhammad (ṣaḥāba) pale Saqifah.
Mtazamo huo kimsingi unapingana na ule wa Uislamu wa Kisunni, ambao wafuasi wake wanaamini kwamba Muhammad hakuteua mrithi kabla ya kifo chake na wanamchukulia Abu Bakr, ambaye aliteuliwa kuwa khalifa na kundi la Waislamu wakuu pale Saqifah, kuwa khalifa wa kwanza halali (rāshidūn) baada ya Muhammad.[3]
Washia huamini ya kwamba familia ya Muhammad hustahili kuwa na uongozi kati ya Waislamu. Familia hii huitwa "ahl-al-bayt" (Kiarabu:أهل البيت).
Ali alimwoa mtoto wa pekee wa mtume aliyeishi yaani binti yake Fatima akawa pia baba wa Hassan na Husain wajukuu wa pekee wa mtume. Baada ya kifo cha Ali wafuasi wake walitaka Hasan na Husein kumfuata katika nafasi ya uongozi wa Uislamu wote lakini idadi kubwa ya Waislamu walishikamana na Muawiya
Washia huamini ya kwamba uongozi wa ahl-al-bayt uliendelea kupitia maimamu mbalimbali.
Washia waligawanyika baada ya imamu wa sita Ismail ibn Dschafar kuhusu swali ni nani imamu halali wa saba. Kutokana na farakano hili vikundi mbalimbali vilijitokeza.
Kutokana na uhamiaji wakati wa karne ya 19 matawi ya Waismaili yamepatikana pia katika Afrika ya Mashariki. Hasa Wakhodja wamejitolea katika mazingira wanapoishi kwa kujenga shule, sahanati na mahospitali vinavyoitwa mara nyingi "Aga Khan".
Kihistoria palikuwa na vikundi vingi vingine kama vile Wafatima waliotawala Misri kati ya 953 na 1171 BK.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.