Sarah Wayne Callies
From Wikipedia, the free encyclopedia
Sarah Wayne Callies (Sarah Anne Callies amezaliwa tar. 1 Juni 1977 huko La Grange Illinois) ni mwigizaji filamu na tamthiliya wa Kimarekani, anayejulikana vizuri baada ya kuigiza kama Dr. Sara Tancredi katika misimu miwili ya kwanza ya tamthilia ya Kimarekani Prison Break.
Wasifu
Miasha ya Awali
Callies na familia yake walihamia Honolulu, Hawaii. Kipindi hicho alikuwa na umri wa mwaka mmoja. Alianza kujionyesha mapema kuwa mapenzi yake ni kuigiza kwa kushiriki katika maigizo kadha wa kadha ya shuleni hapo Punahou School.
Wazazi wake wakiwa ni maprofesakatika chuo cha Hawaii kilichopo Manoa, Callies hakufuata nyayo zao kabisa. Badala yake, alichagua kujiingiza moja kwa moja kwenye Uigizaji. Alipohitimu elimu ya sekondari, alijiunga na chuo cha Dartmouth kilichopo Hanover, New Hampshire. Pamoja na kuwa na masomo, aliendelea kujihusisha kwenye maigizo.[1] Aliendeleza elimu yake hapo Denver's National Theatre Conservatory alipojipatia Shahada ya Sanaa ya Maigizo hapo 2002.[1]
Sanaa
Callies's alionekana mara ya kwanza kwenye luninga kama Kate O'Malley, uhusika wa mara kwa mara kwenye Queens Supreme. Aliigiza nafasi ya nyota kwa mara ya kwanza kama Jane Porter kwenye tamthiliya ya Tarzan, iliyorushwa na Warner Bros.
Baada ya kushirikishwa kwenye Law & Order. Special Victim Unit, Dragnet na NUMB3RS, Callies alikamata nafasi ya nyota kwenye Prison Break ya FOX kama Dr. Sara Tancredi. Pia aliigiza kama nyota kwenye filamu za Universal Picture za Whisper na The Celestine Prophecy.
Maisha Binafsi
Mnamo Juni 21, 2002, Callies alifunga ndoa na Josh Winterhalt, aliyekutana nae katika chuo cha Dartmouth. Winterhalt ni mwalimu wa sanaa. Ilipofika Januari 23, 2007, msemaje wake alitangaza kuwa wawili hao walikuwa wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza. Julai 2007, Callies na mume wake walimkaribisha mtoto wao wa kike, Keala Winterhalt(Kay-AH-lah).[2][3]
Maigizo
Filamu
Tamthilia
Marejeo
Viungo Vya Nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.