From Wikipedia, the free encyclopedia
Sanje ni kata inayopatikana katika tarafa ya Kidatu, wilaya ya Ifakara Mjini, Mkoa wa Morogoro, Tanzania yenye Postikodi namba 67507.
Kata ya Sanje ipo kando ya safu za Milima ya Udzungwa na ina vivutio vya utalii ambavyo baadhi yake vinavyopatikana katika milima hiyo kama vile maporomoko ya maji ya Sanje (Sanje Waterfalls) na wanyama jamii ya nyani wanaofahamika kama mbega.
Kata hiyo inajumlisha vijiji vitatu ambavyo ni Sanje, Msolwa Ujamaa na Miwangani. Jina la kata limetokana na uwepo wa kijiji cha Sanje chenye vitongoji kama Shuleni, Barabarani, Mpirani na Udzungwa.
Kadiri ya sensa ya mwaka 2022 kata ina jumla ya wakazi 12,777 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 11,041 [2] walioishi humo.
Wakazi wa kata hiyo hujishughulisha zaidi na kilimo cha mazao ya biashara kama miwa kwa wingi ambayo waiuza katika kiwanda cha miwa cha Kilombero Sugar Company Limited, na mpunga. Pia hulima mazao mengine kama mahindi na viazi vitamu.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.